Monday, May 17, 2010

ITS A WTISD(World Telecommunication & Information Society Day

WTISD 2010 Poster


baadhi ya watanzania waliohudhuria washa hiyo wakiingia kwenye uwanja wa Expo Shanghai 2010. Kushoto ni Dr. Justinian Anatory (Mjumbe wa Bodi ya TCRA) akiongozana na Dr. Joseph Kilongola (Mkurugenzi wa TEKNOHAMA TCRA).
mabanda mbalimbali ya maonesho ya nchi mbalimbali zinazoshiriki kuonesha jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano inavyoweza kuboresha miji duniani na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Tarehe 17 ya Mwezi mei kila Mwaka, Dunia huadhimisha siku ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Jamii (TEKNOHAMA). Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano Duniani, International Telecommunications Union (ITU), huadhimisha siku hii muhimu kwa nia ya kukumbushana umuhimu wa teknologia ya habari na Mawasiiano kwa maendeleo ya dunia na jinsi inavyoweza kuboresha maisha ya wanadamu kwa ujumla.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa kimataifa katika jiji la Shanghai nchini China ambako maonesho makubwa ya teknolojia yanafanyika kwa kipindi cha miezi sita. Maonesho hayo maarufu kama Expo Shanghai 2010, yanayoendana na kauli mbiu ya mwaka huu, "Miji Mizuri, Maisha Bora" yalianza rasmi mei mosi mwaka huu na yataendelea hadi mwezi October 2010. Bofya hapa kwa habari zaidi: http://www.itu.int/wtisd/2010/theme.html
Mamilioni ya watu wamefurika kwenye jiji hili la Shanghai linalokadiriwa kuwa na wakazi milioni 22 na ushee katika kusheherekea maadhimisho haya yatakayofikia kilele jumatatu tarehe 17 Mei 2010 kwa hotuba na makongamano mbalimbali yanayolenga katika kuelezea mafanikio ya sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mchango wake katika kuboresha majiji na miji ili kuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi.
Watanzania kadhaa wako mjini hapa kushiriki katika maadhimisho haya yaliyopata baraka za ufunguzi na Mama Anna Tibaijuka, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (HABITAT).
Jana katika Banda la Umoja wa Mataifa, ITU ilifanya washa kuhusu umuhimu wa TEKNOHAMA katika kuboresha mazingira duniani na hasa katika kujenga "miji kijani" ( ICT's: Building the Green Cities of the Future).
Wataalamu mbalimbali walitoa mada zilizoibua hisia mbalimbali kutoka kwa washiriki hususan mapendekezo ya ITU ya kuwa na charger moja kwa simu zote (Universal Charger). Mada ingine iliyosisimua ni ile ya uchafuzi wa mazingira kwa magari yanayotoa hewa chafu ambapo imependekezwa nchi duniani na hasa majiji yajizatiti kuyaondoa magari yanayoharibu mazingira zaidi.
Bofya hapa kupata mawasilisho ya mada hizo kwa undani.

No comments:

Post a Comment