Sunday, April 25, 2010

WEBSITE YA afroIT YAZINDULIWA CHINA


Ukurasa mkuu wa AfroIT
Mdau akimwaga sera katika hotuba ya uzinduzi wa AfroIT
Mdau akichangia mada katika uzinduzi wa AfroIT

AfroIT crew na baadhi ya wageni waalikwa
Wadau wakifuatilia uzinduzi wa AfroIT


Brother Nyamwese Jr!
Pole na majukumu ya blog ya college yenu. Naomba uwatambulishe wana Informatics mtandao wa


www.afroit.com
ambapo mnamo Ijumaa tar 23 Apr
kulifanyika uzinduzi rasmi wa tovuti yetu
katika jiji la Wuhan hapa China.

1.Utangulizi
AfroIT Group ni kikundi cha Watanzania wachache ambao ni vijana waliojikita kwenye uwanja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) wakiwa na azma ya kuwafahamisha, kuwaelimisha na hata kuwajulisha Watanzania masuala mbalimbali yahusuyo ICT kupitia njia ya mtandao(yaani kupitia tovuti yetu ya www.afroit.com).

2.Azma
Kama nilivyodokeza hapo awali, azma yetu hasa ni kutoa ufahamu na elimu kwa ndugu zetu watanzania katika uwanja wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Kwa mantiki hii, tunaamini AfroIT inaweza kuwa msaada kwa jamii nzima kuanzia wanafunzi hadi wananchi wa kawaida mwenye kiu na uhitaji wa nyenzo muhimu ktk ICT.

3.Kilichomo AfroIT
Ndani ya tovuti yetu, kuna kurasa mbalimbali ambazo tumezigawanya ktk makundi matano ambayo ni "e-learning", "technology", "forums", "blog" na "downloads".Hivyo basi kupitia kurasa hizi :

utaweza soma vijarida na vitabu mbalimbali
kuangalia video mbalimbali za masomo
kuuliza yale yanayokutatiza na kuchangia mada mbalimbali
kupakua(kudownload) vitabu mbalimbali kwa urahisi
kukutana na habari mbalimbali zinazojiri katka ulimwengu wa ICT

Hivyo basi ni tumaini letu kuwa ndugu zetu Watanzania mtauthamini mchango wetu na tunategemea kuungwa nanyi mkono katika ushauri, mawazo na hata kukosolewa inapobidi.

Kwa ushauri, maswali au maoni wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo:
info@afroit.com
au
webmaster@afroit.com

Tembelea www.afroit.com leo kwani "elimu ni ushindi"

WANA INFO HII NI CHANGAMOTO TUICHUKUE.

No comments:

Post a Comment